YESU ANAWAFUNZA WANAFUNZI WAKE
YESU ANAWAFUNZA WANAFUNZI WAKE
(a) Sifa za Heri—Picha ya mtakatifu "Akafunua kinywa chake na kuwafunza"
Baada ya majaribu ya nyikani, Yesu alirudi Galilaya “kwa nguvu za Roho. habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando” (Lk. 4:14).
Sura nne ya Mathayo (Mst. 12-25) ina kumbukumbu ya kazi ya kina ya
mahubiri ya Galilaya, ambapo mafunzo na miujiza ya uponyaji ulivutia
“umati mkubwa” kutoka sehemu za kaskazini mwa Galilee na Dekapoli, na
kutoka mbali hadi Yerusalemu, Yudea na ng’ambo ya Yorodani. Wakati Yesu
aliona umati huu alipanda juu ya mlima na pale akaelezea kuhusu sifa ya
maadili ya wale wanaostahili ufalme wake. Lengo letu katika somo hili ni kuona tabia ambayo tunapaswa kuendeleza.
Mathayo 5:1-12
MMOJA ALIYE MKUU KULIKO MUSA
Yesu na Musa walipanda milimani na kutoa sheria ya Mungu kwa watu
wake. Lakini Yesu alikuwa mkuu. Wakati Musa alikuwa mpatanishi ambaye
"alipokea sheria iliyoletwa kwake na Malaika" (Gal 3:19;
Mdo. 7:38, 53), mawasiliano ya Mungu kupitia Yesu yalikuwa ya moja kwa
moja. Yesu “alifunua kinywa” na maneno ya Mungu yakatoka (Ebr 1: 1-2;
Kum. 18: 15-19; Mdo 3: 22-23). Tena, ambapo sheria ya Musa ilioredhesha
baraka kwa na laana kwa wale wakaidi (Kum. 28), Yesu aliongea kuhusu
baraka pekee. Baadhi ya watu wamehususha hili kwa upole, lakini kinyume
chake ni kweli. Wakati wakaidi waliishi chini ya laana ya katiba ya
Musa, hawa wataondolewa na Yesu. Hawatafikiriwa. Watatengwa wakati wa
mwanzo wa utawala wake (Mt.. 7:23).HERI NJEMA
Utu ambao Yesu alielezea katika heri njema ("Baraka" ya Mt. 5: 3-11) kimsingi ni zake mwenyewe, lakini zingine zilitabiriwa., kwani aliongea kuhusu “hao”, “wao” na “ninyi”. Tabia hazikupaswa kuonyeshwa moja kwa moja katika watu tofauti, lakini kuonyesha tabia ya utu wa jumla. Aidha, Hotuba aina uhusiano wowote na wale walio nje ya Imani ya Israeli. Inaonyesha maadili ya watu walio TaYARI ndani ya agano na Mungu. Lakini, katika Heri, Yesu anaelezea pande mbalimbali za tabia yake, pia alielezea MAENDELEO ya tabia hio, na kutokana na hilo, maendeleo ya tabia yoyote ingefananishwa na yake. Katika kila ya heri nane, mtu anayeongea kumhusu anasemwa kuwa “Heri”- au furaha - si tu kwa sababu ya matarajio yaliyowekwa mbele yake, lakini kwa sababu ya utulivu wa kuendeleza akili ya wale wanaojua na kufanya mapenzi ya Mungu (linganisha. Yohana 13:17). Tena, katika Heri ya kwanza na ya mwisho, imesemwa kwamba heri ni kwa wale “ufalme wa mbiguni ni wao”. Hii haimaanishi kwamba wako tayari kwenye ufalme wa Mbiguni. Hali milikishi ya sasa inatunika kwa sababu watu wa Mungu wameunganishwa na agano la Ufalme. Darasa hili haliwezi kushindwa kufikia hilo. Ufalme unasemekana kuwa “wa Mbiguni” kwa sababu utakuwa Ufalme wake yule mwenye enzi Mbiguni na utaongozwa na kanuni zake.
Zifuatazo ni heri nane njema-
- Heri walio maskini wa roho; Mt. 5: 3 linganisha. Isa. 66: 2. Jambo muhimula kwanza ni umaskini wa roho. Akili kama hii imekataa yote ambayo mwili unaona kuwa ya kuvutia. Chaguo lazima lifanywe. Mtu hawezi kusafiri barabara mbili ambazo zinaelekea mahali tofauti. Mtu hawezi kuanza kukubali zawadi za Mungu mpaka pale atakapokuwa tayari kukataa zawadi ambazo dunia inampa. Mtu lazima akatae maarifa ya binadamu, na “anyenyekee kwa Neno”. Lakini mwishowe wa “umaskini” huu au kukataa mambo ya dunia na njia zake, kuna utajiri mkubwa- nafasi ya milele katika Ufalme wa Mungu.
- Heri walio na huzuni- Mt. 5:4; linganisha. Isa. 61:3: Haya ni matokeo ya kawaida ya roho iliyokataliwa. Kwa wale wanaopunga mkono wa “kwaheri” kwa yale ulimwengu unawapa, wana matumaini kwamba yametatuliwa, watu hawa wanahusishwa na Ukweli. Wanatazama ulimwengu kutoka kwa mtizamo wa Mungu, na wanaomboleza janii ambayo aidha haina haja, au inayopinga mambo ya Sayuni. Maneno ya Kristo yametoka katika kitabu cha Isaiya 61:3, ambapo wale wanaoomboleza wanasemekana “kuomboleza Sayuni”. Wanaomboleza kukosekana kwa Bwana wao (Mt. 9:15), Na wanasubiri “nyakati za kuburudishwa” kama zilivyotajwa katika Matendo 3: 19-21.
- Heri walio wapole- Mt. 5:5; linganisha. Zab. 25:9-14; 37:11. Ni wasikivu- wanaweza kuundwa katika mikono ya Mfinyanzi “walio wapole atawaongoza kwa hukumu: walio wapole atawafunza njia zake”. Kwa dunia wao ni dhaifu na wasio na ladha, lakini tabia hii inapatikana kwa wale walio na tabia dhabiti (mfano Musa-Hes 12: 3) na zawadi ya kukataliwa ambayo ujasiri na kujizuia kunahitajika. Hawana imani na mwili, lakini wanafurahia katika Neno na kuiga maagizo yake (Flp.3.3)
- Heri wenye njaa na kiu ya haki--Mt. 5: 6; linganisha. Isa. 55: 1. Kupata maisha kwa kuyacha yaende ni utaratibu wa bure. Unawapokonya mitume kiungo kinachowapa hali ya kuridhika kwa akili. Lakini maisha hayawezi kubaki bila chochote. Mtu ambaye anatoshelezwa na dunia na hana haja na chakula cha kiroho Aliye maskini wa roho, mpole, nk, heri kwa sababu ya sifa walionazo tayari, lakini Kristo habariki “wenye haki” aidha, anajua wale ambao wana tamaa ya dhati na haki- wakitamani kuona siku ile ambayo haki ya Mungu itaonekana ulimwenguni na, isitoshe haja ambayo hata sasa, tabia yetu na matendo yanaweza onyesha haki ya Mungu Petro akasema: “kama watoto waliozaliwa wanatamani, maziwa ya dhati ya neno, ili mpate kukua na kukombolewa "(1 Pet 2: 2). Ni katika Neno tunapopata kuridhika kwa njaa yetu ya haki, "Mimi ni mkate wa uzima" Yesu alisema, “yeyote atakaye kuja kwangu hataona njaa; na yeye aniaminiye mimi hataona kiu kamwe" (Yohana 6:35, 7: 37-38).
- Heri walio na huruma- Mt. 5: 7; linganisha. Zab. 18:25. Haki inawakilisha kipengele kikali cha tabia inayofaa. nidhamu kali inaweza kuleta mtazamo mkali kwa mapungufu ya wengine. “Ukali" Lazima utoshanishwe na "Wema" kama ni katika Bwana mwenyewe (Rom 11:22 linganisha Kut. 34: 6-7). hakuna kitu kinacho tia mtu roho kama haki iliyo na huruma na rehema? “Upendo wa Mungu” pale tunapoujua kwa rehema yake na ukarimu wake, unajenga ndani yetu upendo na tamaa ya kufanya jambo kwa yule aliye fanya mengi kwa ajili yetu (linganisha Lk 11:42, 2 Kor.5:14; Mt. 23:23). Mapenzi ya Mungu yanaonekana katika mapenzi ya watu wake. Hatuwezi kutoa kama Mungu, lakini tunaweza na tunapaswa kujifunza kusamehe kama Yeye, na kuwa na Huruma. Tabia hii inapatikana kwa wale ambao ni watiifu kwa amri kuu ya pili (Mt. 22:39; linganisha Yak 2: 8-13).
- Heri kwa wale walio na roho safi- Mt. 5: 8; linganisha. Zab. 24: 4-5; 18:26. Tabia bado haijakamilika. Tunageukia kwa Makini kwa roho. Ni pale tu moyo wetu uko safi, maisha yetu hayawezi kuwa, lakini matendo mengi na maneno yanaweza kuonekana kuashiria hilo (Tit. 1:15). "Safi" inamaanisha “isiyo changanywa” Mungu ni msafi bila mchanganyiko. Yesu hafikirii kuchanganya hali ya uchafu. Roho sio safi kama tamaa za mtu za kibinafsi zimechanganyika na za Mungu. Lakini kwa kawaida, “moyo ni mdanganyifu na zaidi ya hayo ni mwovu” (Yer.17: 9). Kwa jinsi gani tunaweza takaswa? Kwa kuendeleza hatua za Heri na kujitolea kwake kwa dhati kwa yule aliye Msafi, na Mtakatifu. Ni hivyo tu tunaweza “Kuona uso wake”, kumaanisha kukubalika katika Uwepo wake na kufanywa “kama yeye” kimwili. Tizama mawazo sawia katika 1 Yn. 3: 1-3 na Waebrania. 12:14.
- Heri wapatanishi- Mt. 5: 9. Ubora huu ni matokeo ya tabia kamilifu. Kabla mtume aweze kufanya amani, lazima atulize roho yake inayohangaika (linganisha Zab. 16:32. 25:28). Amani ni moja katika ya matunda ya roho mtakatifu (Gal. 5:22). Yakobo anarejelea mawazo ya Yesu wakati anasema kwamba “ Maarifa yatokayo mbiguni, kwanza ni safi, tena ni ya amani". Kinyume chake ni kweli kwa wale ambao wana wivu, chuki na ubinafsi katika nyoyo zao (Yak 3: 14-18). Ilio safi Inaleta amani, wanajenga na kuwanganga wale walioumia (Isa. 58:12). Ni vigumu kudumisha amani ile ambayo “imetengenezwa” “kutafutwa” na kutamaniwa kwa dhati (Yak 3:18; Zab. 34:14; Efe 4: 3). Wapatanishi ni “Wana wa Mungu”. Wanaonyesha kiwango ambacho Yesu, ndungu yao mkubwa ni mkuu milele (linganisha Efe. 2: 4; Rum 5: 1; Isa 9: 6).
- Heri wanaoteswa kwa ajili ya haki- Mt. 5: 10-12; linganisha. Isa. 66: 5.Tabia ya watakatifu si ya kuvutia kwa ulimwengu. Mitume wa Yesu wangekumbana na mateso kama yake na kupitia chuki na unyama pamoja naye. Kipimo cha imani yao kingekuwa kipima cha mateso yao. Mateso yangeendeleza uaminifu na nguvu ya tabia. Wao, pia, watafanywa “dhabiti kupitia mateso” (Ebr 2:10; 5: 8-9). Tazama hasa katika mstari wa 10 na 11 kwamba “ kwa ajili ya haki” ni sawa na “kwa ajili yangu”. Ndani ya Yesu haki ya Mungu inatangazwa. Katika maneno anayo ongea mwenyewe: “Heri ni kwenyu nyinyi”. Walikuwa wale ambao wangepeleka jina lake kwa ulimwengu na wangeteseka kwa hilo (1 Kor 4: 9-13). Hata hivyo mateso yao yangewatoshanisha na Yesu na manabii. Hii ingewapa motisha, kwani wangekuwa wameahidiwa zawadi ya Ufalme. Badala ya kuwa na huzuni, walikuwa na sababu ya kuruka kwa furaha (linganisha Mdo. 05:41; 1 Pet 4: 13-14; 3:14; Flp. 1:29).
MAMBO TUNAYOJIFUNZA:
- Tabia zilizo wekwa wazi katika Heri ni zile za mtu kamili wa Mungu anayepatikana katika Bwana Yesu Kristo mwenyewe.
-
Aidha, inaelezea mchakato ambapo mtu hukua, hatua kwa hatua katika kutafuta kufikia mfano wa Kristo.
• Hatua hizi ni: -
1) kuikana dunia;
2) Kuomboleza kwa ajili ya Sayuni ya ukamilifu,
3) Usikivu - utayari wa kupokea Neno la Mungu,
4) Hamu ya njia za Mungu kuzingatiwa, na kudhihirishwa,
5) Kuwa tayari wa kusamehe-kama ukali lazima uwe na uwiano na wema;
6) Motisha wa kweli wa ndani ya moyo usio changanyika, usiogawanyika katika uaminifu wake, ambapo Mungu ako huru kuingia, ndani yake. Yeye anaweza kuonekana.
7) Mtu, mwenyewe ametengenezwa na kutengwa na dhambi, ambaye anataka kurejesha, au kurekebisha, wengine.
8) Tabia, dhaifu na haitoshi kwa viwango vya duniani, lakini ambayo ni upinzani wake wa dunia, na kwa ajili ya mtu anayetarajia kuteseka, kama Kristo alivyofanya. Mizizi ya heri hupatikana katika udongo wa Agano la Kale. Katika kauli hizi fupi kupatikana kiini cha manabii- Tumaini la Israeli.
No comments:
Post a Comment